Bunge
la Gambia limeongeza muhula wa Rais wa Gambia Yahya Jammeh ambao
unakamilika siku ya Alhamisi kufuatia kushindwa kwake kwenye uchaguzi
kwa siku 90.
Bunge pia limeidhinisha uamuzi wa Jammeh wa kutangaza hali ya tahadhari ya siku 90, katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi.
Viongozi wa kanda wametishia kutumia nguvu za kijeshi kumlazimisha bwana
Jammeh kuondoka madarakani, ikiwa atakataa kusalimisha mamlaka kwa rais
mteule Adama Barrow.
Maelfu ya watalii raia Uingereza na Uholanzi wanaondolewa kutoka Gambia.
Nchi hiyo ni maarufu kwa watalii kutokana na fukwe zake.
Gambia ilitumbukia kwenye mzozo baada ya bwana Jammeh kukataa ushindi wa
bwana Barrow kwenye uchaguzi wa tarehe mosi mwezi Disemba.
Viongozi wa kanda wameshindwa kumshawishi Bwana Jammeh kuwacha madaraka.
Nigeria imetuma meli ya kivita kumshinikiza bwana Jammeh kuondoka madarakani.
Muungano wa nchi za magharibi mwa Afrika Ecowas, umeandaa kikosi
kinachoongozwa na Senegal lakini bado unasema kwa hatua za kijeshi ndizo
zitakuwa za mwisho.
No comments:
Post a Comment