Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimia na Mwenyekiti
wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki
(CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh alipowasilia katika Chuo cha KumbuKumbu ya
Mwalimu Nyerere katika kongamano la Lugha ya Kiswahili.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimia na Waziri
zamani wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Mohamed Seif Khatib wakati
alipowasili katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere kufungua
kongamano la Lugha ya Kiswahili.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akiweka saini katika
kitabu cha wageni mara alipowasilia katika Chuo cha KumbuKumbu ya
Mwalimu Nyerere katika kongamano la la Lugha ya Kiswahili.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati) akielekea
katika Ukumbi wa Utamaduni katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere
kufungua kongamano la Lugha ya Kiswahili. kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo
cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere( Mipango Fedha na Utawala) Dkt.
Magreth Shawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi wa
Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh
Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Shani kitogo akiimba
ushairi katika ufunguzi wa kongamano la la Lugha ya Kiswahili
liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni
Jijini Dar es Salaam.
Bw. Sarungi Innocent akisoma
risala kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia James Wambura(hayupo Pichani) kwa niaba ya Chama cha
wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) wakati wa
ufunguzi wa kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo
cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akipokea Risala kutoka kwa
Bw. Sarungi Innocent aliyesoma risala kwa niaba ya Chama cha wanafunzi
wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) wakati wa ufunguzi
wa kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha
KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mlezi wa Chama cha wanafunzi wa
Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) na Waziri zamani wa
Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Mohamed Seif Khatib akitoa mada
mbalimbali kuhusu Lugha ya Kiswahili katika kongamano la Lugha ya
Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere
Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mwandishi mashuhuri wa vitabu vya
Riwaya Bw. Shafi Adam Shafi akitoa mada mbalimbali kuhusu Lugha ya
Kiswahili katika kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika
Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi
wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh
akitoa maelezo kuhusu Chama chake katika kongamano la Lugha ya Kiswahili
liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni
Jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkuu wa Chuo cha KumbuKumbu
ya Mwalimu Nyerere (Mpango Fedha na Utawala) Dkt. Magreth Shawa akieleza
kuhusu Chuo chake katika kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika
katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akizungumza na washiriki
wa kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha
KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akipongezwa na Mwandishi
mashuhuri wa vitabu vya Riwaya Bw. Shafi Adam Shafi mara baada ya
kumaliza kuzungumza na kufungua rasmi kongamano la Lugha ya Kiswahili
liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni
Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia
mambo mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika katika kongamano la Lugha ya
Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere
Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakiangalia
vitabu mbalimbali katika maonesho ya vitabu yaliyofanyika sambamba na
kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu
ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Serikali kupitia Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo imeanza rasmi kuandaa Sera ya Lugha ambayo
itatoa muongozo kwa taifa kuhusu masuala yote ya maendeleo ya Lugha
nchini ikiwemo Lugha ya Taifa ya Kiswahili.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura wakati
akifungua kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha
KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Anastazia Wambura amesisitiza
kuwa kwa kipindi kirefu sana kumekuwa na uhitaji wa Sera ya Lugha
ambayo itasaidia katika ukuaji na matumizi sahihi ya Lugha hasa Lugha ya
Taifa ya Kiswahili.
“Kwa hivi sasa rasimu ya awali
imeandaliwa na tunaendela kupokea maoni kutoka kwa wadau na kuyachambua”
Alisistiza Mhe. Anastazia.
Ameeleza kuwa Sera ya Lugha
itasaidia Lugha za Asilia, Lugha za alama , maandishi ya nukta nundu na
Lugha za kigeni kuwekewa mkakati wa kuzishughulikia na kuzitumia kwa
kukidhi mahitaji ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi
Shani kitogo ameeleza kuwa mchakato wa kupokea maoni unaendelea na
amewaomba wadau wa Lugha hasa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili kuendelea
kutoa maoni yao kwa ajili ya kupata Sera ya Lugha iliyo bora na
itakayosaidia katika maendeleo na ukuaji wa Lugha nchini.
“Niwaombe wadau wa Lugha nchini
waendelee kuleta maoni yao kwetu ili kuweze kufanikisha kupata Sera ya
Lugha kwa Maendeleo ya Taifa Letu” Alisisitiza Bibi Shani.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha
wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw.
Byatato Awadh ameishukuru Serikali ya waamu ya Tano kupitia Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha
wadau wa Lugha kwa kuanza kuandaa Sera ya Lugha itakayoleta maendeleo
katika ukuaji wa Lugha nchini.
“ Niishukuru Serikali ya Awamu ya
Tano kwa kuwa sikivu kwa wananchi na wadau wa maendeleo na tunaahidi
kutoa ushirikiano katika uandaaji wa Sera hii ya Lugha”Alisisitiza Bw
Byabato.
No comments:
Post a Comment