Na: Lilian lundo – MAELEZO
Serikali ndiyo yenye mamlaka ya
kutangaza ikiwa nchi inakabiliwa na janga la njaa na wala si taasisi,
asasi za kiraia au wanasiasa.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa
Chama cha UDP John Cheyo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii
alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu mijadala mbalimbali inayoendelea
katika vyombo mbalimbali vya habari kwamba Tanzania imekabiliwa na
tatizo la njaa.
Cheyo alisema kuwa, huwezi kusema nchi ina njaa wakati vyakula vipo katika masoko mbalimbali hapa nchini.
Amewataka watanzania kutofautisha kupanda kwa bei za vyakula na janga la njaa.
Aidha, Cheyo alisema kuwa tatizo
hilo tayari limetatuliwa na Serikali kwa kutoa tani milioni 1.5 za
mahindi ambazo zitasambazwa nchi nzima kwa ajili ya wananchi kununua.
Aliendelea kwa kusema kuwa kuna
umuhimu mkubwa wa mahindi hayo kuuzwa kwa uangalifu kwani gharama yake
itakuwa ni ya chini, hivyo kuna watu ambao watajitokeza kununua kiasi
kikubwa na kwenda kukihifadhi kwa ajili ya kukiuza kwa gharama ya juu
baadae.
Vile vile aliwataka watanzania
kuwa na tabia ya kutunza vyakula badala ya kuuza vyakula vyote mara
wanapovuna, ili vyakula hivyo viweze kuwasaidia pale ambapo mvua
zinakuwa zimechelewa kama ambavyo imekuwa kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment