Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kulia), akitoa maelekezo kwa Mjumbe
wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF Bw. Godfrey Simbeye,
wakati alipokagua shughuli zinazofanywa na mfuko huo jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kulia), akipata taarifa ya utendaji
kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF Eng.
Peter Ulanga, alipokagua shughuli zinazofanywa na mfuko huo jijini Dar
es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kumbukumbu za wateja
wanaohudumiwa na kampuni ya simu TTCL kanda ya Kaskazini eneo la
Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akisisitiza jambo kwa
maofisa wa kampuni ya Simu TTCL kanda ya Kaskazini alipokagua huduma
zinazotolewa na kampuni hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa ofisa
wa kampuni ya Simu TTCL namna ya kufanya kazi kwa ubunifu ili kuongeza
wateja katika kampuni hiyo.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Mfuko wa
Mawasiliano kwa wote (UCSAF), kuhakikisha vijiji vyote nchini ambavyo
havijaunganishwa na huduma ya mawasiliano vinaunganishwa kabla ya
mwisho wa mwaka huu.
Aidha, Profesa Mbarawa amesisitiza
mfuko huo kutoa kipaumbele kwa vijiji vyote vilivyomo sehemu za
mipakani ili kuimarisha ulinzi na uharaka wa mawasiliano katika maeneo
hayo.
Amewaagiza UCSAF kukutana na
mitandao ya simu ili kukamilisha kazi kwa mujibu wa mkataba kwa kata
121 ambazo hazijapata huduma ya mawasiliano hapa nchini.
“Nia ya Serikali ni kuhakikisha
vijiji vyote nchini vinapata huduma ya mawasiliano ifikapo mwishoni mwa
mwezi Novemba ili kuwezesha mikakati mingine ya kuboresha Mifumo ya
Tehama katika shule na Hospitali kuendelea na hivyo kuhuisha huduma za
Tehama katika Sekta za afya na elimu”, amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa ameonya kampuni za
simu zitakazoshindwa kupeleka mawasiliano katika maeneo waliyopangiwa
kwa wakati zitapokonywa masafa katika maeneo husika ili kuzipa kampuni
zilizo tayari.
Naye Mjumbe wa Bodi ya UCSAF Bw.
Godfrey Simbeye, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga
kuhakikisha inaratibu huduma zote za Tehama zinazotolewa na taasisi
mbalimbali nchini ili kuweka uwiano wa huduma hizo nchini kote.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa
UCSAF Eng Peter Ulanga, amesema kuwa mfuko huo umejipanga kupeleka
mawasiliano katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara ili kutoa haki kwa
wakazi wa maeneo hayo kunufaika na fursa za mawasiliano na kuchochea
maendeleo.
Takribani asilimia 94 ya Wakazi wa
Tanzania wanapata huduma ya mawasiliano lengo likiwa ni kufikia
asilimia 100 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment