Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa maelezo kwa
Wadau wa masuala ya Ujenzi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo wa
kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara
uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa maelezo kwa
katika Wadau wa masuala ya Ujenzi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa
mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wananwake katika kazi za
barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es
salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua
kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi
za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar
es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua
kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi
za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar
es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua
kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikihwaji wa wanawake katika kazi
za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi wa barabara Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng Ven Ndyamkama akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari kuhusu mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa
wanawake katika kazi za barabara,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga katika picha ya
pamoja na wajumbe wa maendeleo ya sekta ya ujenzi mara baada ya kuzindua
kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika
kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa
jijini Dar es salaam.
Picha na Wizara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Imeelezwa kuwa sababu za kihistoria, mila
na desturi za jamii ni moja ya changamoto zinazoikabili sekta ya ujenzi
kwenye ushirikishaji wa wanawake katika utekelezaji wa miradi ya
barabara nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wizara
ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi ),Eng. Joseph
Nyamhanga wakati akizindua mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa
wanawake katika kazi za barabara ambapo Serikali imekuja na mikakati
mbalimbali ya kuwashirikisha wanawake katika miradi ya ujenzi wa
barabara
“Maandalizi ya mwongozo huu ni sehemu ya
mkakati wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika utekelezaji
wa mikakati mbalimbali iliyojiwekea ili kuinua maisha ya wanawake
kiuchumi,” amesema Eng. Nyamhanga.
Eng. Nyamhanga ameongeza kuwa utekelezwaji
wa mwongozo huo ni moja ya kichocheo cha kuwawezesha wanawake kutoa
mchango mkubwa zaidi kuchumi nchini ambapo kwa sasa sekta ya ujenzi
inachangia asilimia 13.6 kwenye pato la Taifa.
Aidha ametanabaisha kuwa kwa mwaka 2014/15
kumekuwa na ongezeko la ushiriki wa wanawake katika miradi ya barabara
wa uwiano wa kila wahandisi 100 wanaume wanawake 6 ambao kwenye
usimamizi wa miradi uwiano ukiwa ni asilimia 6.
Kwa upande wake MKurugenzi wa Idara ya
Barabara, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Ujenzi,
Eng. Ven Ndyamukama amesema ushirikishwaji wa wanawake katika sekta ya
ujenzi ulianza mwaka 1992 kwa kutekelezwa kwenye mikoa ya Mbeya, Tanga,
Shinyanga, Mwanza na Mtwara.
“Kama Wizara tuliona umuhimu wa kuanzisha
kitengo maalum kwa ajili ya kuhakikisha tunawawezesha wanawake katika
kazi za ujenzi na hili limesisitizwa hata kwenye sheria ya Ujenzi ya
mwaka 2003 (CIP, 2003) kwa kuhakikisha wanawake wanashirikishwa katika
kazi za ujenzi ili kuwainua kiuchumi’ amesema Eng. Ndyamukama.
Ameongeza kuwa pamoja na mwongozo huu
Wizara imeendelea kuwawezesha wanawake kwenye mafunzo mbalimbali ya
ujenzi kupitia vyuo mbalimbali vilivyo chini ya wizara na taasisi
binafsi.
Takwimu Kutoka Bodi ya Usajili wa
Wahandisi nchini (ERB) na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB)
zinaonesha kwa mwaka 2014, kati ya jumla ya wahandisi 13,148 waliopo
nchini wahandisi wanawake ni 926 ambao ni sawa na asilimia 6.5 wakati
kati ya Makampuni ya makandarasi 8,071 yaliyosajiliwa ni makampuni 253
yanamilikiwa na wanawake sawa na asilimia 3.
No comments:
Post a Comment