Thursday 19 January 2017

Jengo la Ghorofga 17 laporomoka


Rescue workers gather in front of the collapsed Plasco building in Tehran, Iran (19 January 2017)Wazima moto wengi wanahofiwa kuaga dunia baada ya jengo moja kubwa kwenye mji mkuu wa Iran Tehran, kushika moto na kuporomoka.
Wazima moto 200 walikabiliana na moto huo kwenye jengo hilo la Ghorofga 17 kwa saa kadha, kabla ya kuporoka kwa kwa sekunde chache.
Zaidi ya watu 200 pia nao waliripotiwa kujeruhiwa kwenye mkasa huo.
Waokoaji walifanikiwa kuwaokoa baadhi ya wazima moto
Jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1962, lilikuwa wakati mmoja jengo refu zaidi mjini Tehran.
Moto huo unaripotiwa kuanza mwendo wa saa 04:30 GMT siku ya Alhamisi, wakati watu hawakuwa bado wameingia.
Magari kumi ya kuzima moto yalifika eneo hilo na vituo vya runinga viliripoti kuwa wazima moto kadha walikuwa ndani ya jengo wakati liliporomoka.
Kituo kimoja cha runinga cha serikali kilinukuu afisa mmoja akisema kuwa kati ya watu 50 na 100 wanaaminiwa kukwama chini ya vifusi.
Wazima moto walikuwa wamepambana na moto huo kwa saa kadha



No comments:

Post a Comment