Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akisalimiana na
wananchi wa Kijiji cha Utengule, alipowasili kuzindua ujenzi wa jengo
litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi huku eneo hilo
likitolewa na wananchi wa kijiji hicho.Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya,
Jesse Shengena (kushoto), akimuelekeza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) ramani ya Ujenzi wa
Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika
kijiji cha Utengule wilayani Mbeya. Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Emmanuel Lukula, akitoa maelezo juu ya Ujenzi wa Jengo
litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi kwa Naibu Waziri wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza
kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho cha Utengule wilayani Mbeya.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizindua Ujenzi wa Jengo
litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha
Utengule.Wanaoshuhudia ni baadhi ya mafundi wakiongozwa na Mhandisi wa
Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kulia), eneo la ujenzi wa ofisi hizo
limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji cha
Utengule wilayani Mbeya.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Utengule baada ya kuzindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika
kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule
wilayani Mbeya.Naibu Waziri aliwashukuru wananchi hao kwa kujitolea eneo
la kujengwa ofisi za watumishi na askari wa jeshi ikiwa ni juhudi zao
katika kupambana na matukio ya uhalifu katika kijiji chao.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment