Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote
Stephen akitoa taarifa ya mkoa na ya vyombo vya usalama wa mkoa huo kwa
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni(kulia), wakati wa ziara ya Naibu Waziri kutembelea idara
zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Wizar ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa, Zelote Stephen mara baada ya kumaliza kupokea taarifa ya mkoa na
ya vyombo vya usalama wa mkoa huo wakati wa ziara ya kikazi mkoani hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza mkoa wa Rukwa kwa ziara
ya kikazi.Kulia ni wakuu wa jeshi hilo mkoani hapo wakimsikiliza.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa,
Kamishna Msaidizi Selemani Kameya akisoma taarifa ya utendaji kazi ya
Mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa,
ACP George Kyando akizungumzia Mradi wa Ujenzi wa ofisi wakati Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya mradi huo na kuwataka
kutumia rasilimali watu ya wafungwa waliopo mkoani hapo ili kuweza
kukamilisha ujenzi huo wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mkoani
hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea risala kutoka kwa
askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Rukwa aliyoisoma kwa niaba
ya wenzake ikiwa na maombi mbalimbali yaliyoelekezwa kwa wizara.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na aliyewahi kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Simiyu, Paul Mzindakaya baada ya kumaliza kupokea
taarifa ya hali ya usalama mkoani Rukwa wakati Naibu Waziri alipokuwa
mkoani humo kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment