Sunday 22 January 2017

Umuhimu wa kuota jua katika miili yetu


Uwezekano wa binadamu wa kuwa na uhakika wa kuishi maisha marefu, hutegemea hatua rahisi na zenye mabadiliko makubwa katika mwili wake. Njia hii itakusaidia wewe uwe na uhakika wa kuwa na maisha imara yenye afya bora.
Ota Jua la Asubuhi kwa dakika 15 kila siku
Toka nje ya nyumba wakati wa jua hasa lile la hasubuhi, kwani jua litachochea seli katika ngozi ya mwili wako na kuzalisha Vitami D.
Inasadikika kuwa asilimia 50 ya watu wazima huwa na upungufu wa vitamini D, kwasababu wengi wetu hatutoki nje kupata mwanga wa jua (sii sahihi kuota mwanga wa jua kupitia dirisha lako la kioo ukiwa nadni ya nyumba, kwani kioo huchuja nguvu yote ya jua na kubakia mwanga dhaifu tu.). Unapaswa kuota jua angalau dakika 15 kwa siku, yani toka nje mwanga ukupige usoni, mikononi, miguu na hata ikibidi vaa nguo nyepesi au nguo zenyekuuweka mwili wazi kiasi ili kuruhusu mionzi ya jua kupenya katika ngozi.

Kama unawasiwasi na kiasi cha vitami D katika mwili wako, basi onana na daktari atakufanyia vipimo vya damu ili kujua kiasi cha vitamini D uliyonayo mwilini kwako. Lakini ni vyema ukazingatia kuota jia kwa dakika 15 kila siku kwasababu jua pia hukusaidia kukupatia mfumo mzuri wa usingizi kupitia muongozo muri wa homoni za mwili zinazofahamika kitaalamu kama 'melatonin' zinazohusika na kudhibiti mzunguko wa usingizi.
Vtamini D ni kitu kinachopatikana bure kabisa, kwani hakina gharama zaidi ya kuota jua kwa dakika 15 kila siku. (Niaibu kupungukiwa na vitamini D mwilini, Ota jua).

No comments:

Post a Comment