Monday, 23 January 2017

Ubalozi wa Marekani kuhamia Jerusalem.

Tokeo la picha la Mahmoud Abbas

Ikulu ya Marekani imesema itaanza mazungumzo kuuhamisha Ubalozi wake nchini Israel kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.
Serikali ya Israel imeupokea uamuzi huo wa Marekani na kusema kuwa ni mwanzo wa Rais Donald Trump kuanza kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa uchaguzi.
Chini ya sheria za Israel, Jerusalem ndio mji mkuu wa nchi, lakini hata hivyo mji huo pia unadaiwa na Wapalestina kwamba ni wao.

Balozi nyingi zimeweka makazi katika mji wa Tel Aviv.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameipinga kwa nguvu hatua hiyo ya kuhamisha ubalozi wa Marekani.
Mapema jana Jumapili, mamlaka nchini Israel zimeidhinisha ujenzi wa nyumba za makaazi 566 kwa walowezi, Mashariki mwa Jerusalem.
Naibu Meya wa mji huo Meir Turjeman amesema sheria sasa zimebadilika kutokana na Rais Donald Trump kuingia madarakani.

No comments:

Post a Comment