Mathew Festing na Papa Francis |
Kiongozi wa kanisa katoliki anayewasaidia raia wa Malta amejiuzulu
kufuatia mgogoro na Vatican kuhusu mpango wa kusambaza mipira ya kondomu
kulingana na kanisa hilo.
Mathew Festing mwenye umri wa miaka 67 alijiuzulu baada ya papa Francis kumtaka kufanya hivyo katika mkutano siku ya Alhamisi.
hatua hiyo inafuatia ufichuzi kwamba tawi la hisani la kanisa hilo huko
Malta lilisambaza maelfu ya mipira ya kondomu katika taifa la Myanmar.
Kanisa katoliki linakataza utumizi wa mipira ya kondomu.Papa Francis alimtaka kujiuzulu na alikubali.
Tawi hilo la Malta lina uwezo mwingi kama ule wa taifa zima. Hutoa
pasipoti, stampu na leseni na pia lina uhusiano wa kidiplomasia na
mataifa 106 ,ikiwemo Vatican.
Ijapokuwa tawi hilo linaonekana kuwa na wanaume pekee, viongozi wake sio wanaume pekee.
Kufikia 2013 wanawake walikuwa asilimia 30 wakijulikana kama Dames.
No comments:
Post a Comment