Thursday 19 January 2017

Jua zaidi pozi la kuweka kidole kimoja

Je, unajuwa kuwa kupiga picha ukiwa umeweka alama ya “amani na upendo” kwa kuonesha vidole viwili kunaweza kupelekea kuibiwa data zako muhimu?
Utafiti mpya wa Taasisi ya Taaluma za Teknolojia ya Japan (NII) unazua mashaka juu ya pozi hili maarufu la kupigia picha, hasa miongoni mwa vijana na wanaharakati.
Hii ni kwa kuwa teknolojia ya kutambua alama za vidole inazidi kukuwa na kutumika katika kuwatambua watu, kama vile ambavyo sasa hutumika kwenye kufungia na kufungulia simu za mkononi, tablet au kompyuta.
Katika ulimwengu wa sasa, ambapo vifaa hivyo vimeundwa vikiwa na kamera zenye nguvu sana na mitandao ya kijamii ikiwa inatumiwa kutuma picha, kuna hatari kubwa sana ya data binafsi za mtu kuweza kuvuja na kuwafikia wengine.
Watafiti wa NII waliweza kunakili alama za vidole kwa kutumia picha zilizopigwa kwa kamera zilizo umbali wa mita tatu kutoka alipo mtu mwenyewe.
“Kwa kuinua tu alama ya “amani na upendo” mbele ya kamera, alama za vidole vyako zinaonekana wazi kabisa,” anasema mtafiti wa NII, Isao Echizen.
Mtafiti huyo alikiambia kituo cha televisheni cha Yomiuri nchini Japan kwamba “data za kwenye alama za vidole zinaweza kutengenezwa tena kwa kutumia miale mikali kwenye picha.”
“Hili hata halihitaji teknolojia ya kiwango cha juu wala ya gharama kubwa sana. Mtu yeyote anaweza kuzinakili alama za vidole,” unasema utafiti huo.

No comments:

Post a Comment