Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisaini daftari la wageni baada
ya kuwasili wilayani Momba Mkoani Songwe, kwa lengo la kutembelea na
kukagua uingiaji na utoakaji wa raia na wageni katika mpaka wa Tunduma
unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia,
Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
Afisa Uhamiaji Mpaka wa Tunduma
akimuelekeza jambo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (katikati), wakati wa ziara ya kutembelea mpaka
huo unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia,
Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma
Irando akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, walipotembelea jiwe (linaloonekana pichani)
linalotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia.Wengine ni Wakuu wa Idara za
Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na Polisi walioambatana na Naibu Waziri
katika ziara hiyo mkoani Songwe.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Wakuu wa Vyombo
vya Ulinzi na Usalama mpakani Tunduma huku akiwaasa kushirikiana kwa
pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia nchini
kupitia mpaka huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia) akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi wa Serikali na Wakuu wa Idara za Uhamiaji,
Magereza, Zimamoto, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Polisi
baada ya kutembelea mpaka wa Tunduma.Ambapo aliwaasa kushirikiana kwa
pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia nchini
kupitia mpaka huo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma
Irando.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment