Saturday 23 December 2017

Vita ya kufunga mwaka kati ya Real Madrid na Barcelona


Leo ni vita ya kufunga mwaka kwenye ligi kuu soka ya Hispania maarufu kama La Liga, nyota wawili kutoka timu mahasamu Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona watakuwa wanawania kufunga mwaka wakiwa na mabao mengi zaidi.
Kwasasa nyota hao wana mabao 53 kila mmoja ambayo wameyafunga ndani ya mwaka huu wa 2017 katika mashindano yote. Wanaingia kusaka mabao mengine ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza mwaka wakiwa na rekodi ya kuwa na mabao mengi zaidi.
Kwa upande wa viwango timu hizo zote zinafanya vizuri pamoja na Real Madrid kuanza vibaya msimu, tayari imeshaanza kurejea kwenye ubora wake haswa ikipewa nguvu na ubingwa wa klabu bingwa ya dunia ilioupata wikiendi iliyopita.
Kuelekea mchezo wa leo utakaopigwa saa 9:00 alasiri, Barcelona ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 42 huku wakiwa wameruhusu nyavu zao kuguswa mara saba tu katika mechi 16 huku Real wakiruhusu mabao 11 katika mechi 15 na wakishika nafasi nne wakiwa na alama 31.

Mechi ya leo ni El Clasco ya 237 katika historia ya timu hizo. Real Madrid imeshinda mara 95 huku Barcelona ikishinda mara 92 na kutoka sare mara 49. Messi ndio mfungaji wa muda wote wa El Clasco akiwa na mabao 24 akifuatiwa na Alfredo Di Stefano mwenye mabao 18 na Ronaldo akiwa na mabao 17.

No comments:

Post a Comment