Thursday 21 December 2017

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Heche

 Related image
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini ameitaka serikali kuwa mfano mzuri kwa kutoa takwimu za ukweli na kwamba takwimu nyingi si za kweli na inapaswa kushughulikiwa.
Mbunge John Heche (CHADEMA) ametoa maoni yake hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa ni siku moja baada ya Rais Magufuli kutoa onyo kwa watu wasiohusika kutoa takwimu kufanya kitendo hicho na kuagiza mamlaka husika kuwashughulikia watu hao.
"Serikali inatakiwa kuwa mfano mzuri kwa kutosema takwimu za uongo, lakini tukianzia kwenye takwimu zinazotolewa kuhusu ukuaji wa uchumi, idadi ya viwanda na mengine mengi nafikiri inatakiwa serikali yenyewe ndio ianze kushughulikiwa kwanza," Heche ameandika.
 Jana Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma aliwataka wananchi kuwa makini na masuala ya takwimu na kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma vimekaza ili hali watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka na kwamba mtu akikosea kutoa takwimu ameichafua nchi.


No comments:

Post a Comment