Tuesday 19 December 2017

Moyes ajisifia uwezo wake wa kufundisha timu


Meneja wa wagonga nyundo wa London West Ham United David Moyes, amesema uwezo alionao kwa sasa anaweza kuifundisha timu yoyote duniani na anataka kuonesha kama ana uwezo huo akiwa na klabu yake ya West Ham United.
Tangu alipoteuliwa  kuwa  kocha wa West Ham United  Moyes, ameisaidia timu hiyo kutoka katika mstari wa timu zinazotakiwa kushuka daraja kwa kutokufungwa michezo mitatu.
"Nina uwezo  wa kufanya kazi hii katika klabu yoyote duniani na nina uhakika nitalifanya hili nikiwa na West Ham," alisema kocha huyo.
Kocha huyo  raia wa Scotland mwenye  umri wa miaka 54, anajaribu kurudisha heshima yake baada ya kufanya vibaya alipoviongoza vilabu vya Manchester United, Real Sociedad na Sunderland.

West Ham kwa sasa iko nafasi ya kumi na tano katika msimamo wa ligi kuu ya nchini England.

No comments:

Post a Comment