Friday 8 December 2017

RC Mghwira ajiunga na CCM

Akihutubia katika mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Mama Anna Mghwira ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi.
Mama Mgwira amesema alikuwa kwenye chama tena mwenyekiti lakini anapenda jinsi chama cha Mapinduzi wanavyopanga mambo yao, yanavyoeleweka ndani ya wanachama na mbele ya umma kwa ujumla.
Amesema akiwa kama mkuu wa mkoa Kilimanjaro anashirikiana na vyama vyote ikiwemo CCM, CHADEMA na NCCR ambavyo ndivyo vyama vikubwa mkoani kwake. Amesema katka vyama vyote, ameona CCM inayobadilika japo anaona juhudi za kila mtu lakini juhudi za mtu anaebadilika huwa ziko tofauti, amesema mtu hakiokoka haami duniani bali anasema amebadilika.

No comments:

Post a Comment