Wednesday 20 December 2017

Rais Magaufuli:Kiama kwa wanaosema vyuma vimekaza kuburuzwa Mahakamani

Rais  Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa watu ambao wanasema vyuma vimekaza na wale ambao wamekuwa wakisambaza takwimu mbalimbali za kupikwa kukamatwa na kuwekwa ndani na baadaye kupelekwa mahakamani.
Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma na kuwataka wananchi kuwa makini na masuala ya takwimu pia amewataka kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma vimekaza ili hala watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka.

"Ukikosea kutoa takwimu umeichafua nchi, takwimu ni kitu kibaya sana ndiyo maana kuna watu wamebobea kwenye takwimu hivyo wananchi tuwasikilize watu wa takwimu asitokee mtu mwingine akatoa takwimu tofauti na zile walizonazo watu wa takwimu. Mtu anasema vyuma vimekaza wakati watu wa takwimu wanasema vyuma vimefunguka watu hawa wanatakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani ili wakajifunze kutoa takwimu huko" alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli ameagiza watu ambao watatoa taarifa zozote ambazo zipo kinyume na takwimu walizonazo watu wa takwimu wafikishwe mahakamani "Mimi ningekuwa hakimu watu wa namna hiyo wangepewa adhabu zote mbili kulipa faini na kufungwa"


Mbali na hilo Magufuli amewataka wananchi na taasisi mbalimbali wakitaka takwimu yoyote ile waende ofisi ya Takwimu na wasithubutu kutoa takwimu ambazo zinapingana na zile zilizopo ofisi ya takwimu.

No comments:

Post a Comment