Wednesday 13 December 2017

Wanajeshi waliokufa Congo kuagwa Kesho

Image result for Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linategemea kuaga Miili ya Mashujaa wetu waliouwawa wakiwa katika Jukumu la Ulinzi wa Amani nchini DRC hivi karibuni.
Marehemu wataagwa rasmi kesho Desemba 14, 2017 kuanzia saa 2 asubuhi  katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Upanga jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt Hussein Mwinyi ataongoza kuaga Marehemu hao. Aidha, wananchi wote wanakaribishwa katika kuaga Miili ya Mashujaa wetu.         
                        
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Desemba 13, 2017.

No comments:

Post a Comment