Wednesday 20 December 2017

Chelsea kumenyana na Fc Bournamouth

Msimu wa sikukuu za Xmass umefika, na kama kawaida kwa wenzetu barani Ulaya huwa katika kipindi hichi ndio kipindi ambacho timu zinakuwa na mechi nyingi sana, leo tuone jinsi timu kubwa EPL zilivyo na ratiba ngumu.

Manchester United, wametoka kucheza Jpili mchezo wa ligi zidi ya WBA lakini kesho wako uwanjani mchezo wa Carbao Cup vs Bristol na siku tatu baadae watwafuata Leicester City kisha siku tatu baadae watarudi nyumbani kuisubiri Burnley na kisha Southampton tar 30, watapumzika tar 31 na ikifika tareh 1 watakwenda Goodison Park kuikabili Everton kabla ya kucheza na Derby Country siku nne baadae.

Manchester City, hii leo watacheza vs Leicester City ugenini baadae Jumamos watawakaribisha FC Bournamouth kabla ya kuwafuata Newcastle siku tatu baadae kisha watapumzika na baada ya siku tatu Dec 31 watawakabili Crystal Palace na watapumzika siku moja kisha tar 2 January watawaalika Watford  na Jan 6 watakuwa Etihad kuwakabili Burnley.
Chelsea, leo Dec 20 wanawakaribisha Fc Bournamouth kisha Dec 23 watawafuata Everton, Dec 26 watawakaribisha Brighton kisha Dec 30 watawakaribisha Stoke City baada ya hapo watapumzika siku 3 kabla ya kucheza mchezo mgumu ugenini vs Arsenal na Jan 6 watamalizia na Norwich.
Arsenal, hii leo watacheza vs West Ham, na kisha siku ya Ijumaa watawakabili Liverpool wakiwa nyumbani, Dec 28 watawafuata Crystal Palace kisha siku ya mkesha wa mwaka mpya watacheza vs West Brom, wataukaribisha mwaka tar 3 January vs Chelsea kabla ya Jan 7 kukipiga vs Nottinghma Fores.

Liverpool, kidogo wana ahueni kwa kuwa hawapo katika michuano ya Carbao Cup hivyo watasubiri hadi Ijumaa watakapoikabili Arsenal na kisha siku nne baadae watawakaribisha Swansea kabla ya tar 30 kuwakaribisha Leicester City na siku ya mwaka mpya watawafuata Burnley kabla ya kuwakaribisha Everton Jan 5.

No comments:

Post a Comment