Ronaldo amefikisha Magoli 200 kucheza Michezo 171 kwa Misimu saba

Na Kalonga Kasati
Jina la Christiano Ronaldo si geni masikio mwa watu wengi wanaofuatilia soka uwezo wake katika kucheza Mpira na Mafanikio yake yalianza huko ureno na baadaye akahamia man United ambapo alipata umaarufu mkubwa sana katika
Ukijaaliwa kipaji, kinachofuata ni
juhudi zako binafsi kuhakikisha unafikia malengo pia ukifikia malengo ya
awali lazima ujiwekee malengo mapya. Kama ilivyokuwa kwa Cristiano
Ronaldo, baada ya kutimiza malengo ndani ya Manchester United akaamua
kutimkia Real Madrid ambako ametimiza malengo hadi yale ambayo hakuwa
amejipangia.
Mfungaji bora wa muda wote Real Madrid
Cristiano Ronaldo amevunja rekodi nyingine akiwa santiago Bernabeu.
Magoli aliyofunga jana dhidi ya Valencia yamefikia 200 akicheza katika
dimba la SANTIAGO BERNABEU baada ya kucheza michezo 171 kwa misimu saba
akiwa Hispania, Magoli 149 ameyafunga akiwa katika michuano ya ligi kuu
Hispania wakati 40 akiyapata michuanao ya UEFA, mengine 10 yakipatikana
kwenye kombe la mfalme yaani Copa de rey huku goli 1 likiwa Super cup.
Ronaldo ameanza safari yake ya kufunga
katika uwanja huo akiifunga Deportivo. Lakini pia amefunga mabao mengi
kwenye mchezo dhidi ya Granada alipopiga goli 5 peke yake msimu
wa 2014/15. Mahesabu yanaonesha kasi ya Ronaldo ya kufunga ni goli 1.6
kwa kila mchezo.
Hapa Tanzania rekodi ya Mohamedi Hussein
“Mmachinga” ya magoli 26 kwa msimu mmoja inabaki kuwa ngumu kuivunja
wakati Ulaya kila mechi watu wanategemea kuvunja rekodi .
No comments:
Post a Comment