Tuesday, 10 May 2016

Hujuma za Baadhi ya Wafanyabiashara wa Sukari nchini

 Na Kalonga Kasati

Nchini Tanzania makadirio ya Jumla ya tani 590,000  za sukari zinahitajika, tani laki nne na Elfu ishirini (420,000) kwa matumizi ya kawaida  na kwa viwandani ni tani laki moja na elfu Sabini (170,000), huku uwezo wa uzalishaji kwa viwanda vya ndani ni tani laki tatu pekee, (300,000) kwa mwaka na kuacha pengo la mahitaji ya tani laki mbili na elfu ishirini (220,000) Ambazo kimsingi inabidi ziagizwe kutoka nje.

Mathalani ukiitazama nchi ya India, kitunguu ni bidhaa muhimu sana kama Sukari Tanzania. Yaani ni karibia kila mlo India wanatumia kitunguu. Kupanda kwa bei ya kitunguu India Mwaka 1980 kuliiangusha serikali madarakani na mwaka 1998 bei ya kitunguu ndio iliamua Uchaguzi wa baadhi ya majimbo. Mwaka 2015 kitunguu kilipanda tena na haraka serikali iliamua kuagiza kutoka Pakistani.

Tukirejea nchini Tanzania kuna viwanda vinne (4) tu vinavyozalisha sukari navyo Ni Kilombero Sugar, TPC Moshi, Mtibwa na Kagera. Ambapo makadirio ya mwaka kwa viwanda hivyo ni;-

1.Kilombero Sugar (tani 120,000)
 2.TPC Moshi ( tani 80,000)
  3.Mtibwa (50,000)
4.Kagera (50,000)

Ni Dhahiri kwamba Tanzania haijitoshelezi na wala haitajitosheleza kwa uzalishaji wa ndani wa sukari kwa muda mfupi, isipokuwa pengo linazibwa na sukari kutoka nje, hatua iliyomfanya Rais JPM kuamua kupiga marufuku uagizaji wa sukari nje ya nchi ili itafutwe njia mbadala, ila wakati likisubiriwa hilo,  imebaini vyanzo vya tatizo la upungufu wa sukari nchini humo.

1.Usafirishaji wa sukari kinyume na sheria. Sukari  zaidi ya tani elfu sitini (60,000) Husafirishwa nje ya nchi bila kujali wakati wakijuwa kiwango cha sukari nchini hakitoshelezi  Mahitaji ya watumiaji.

2.Utoaji holela wa vibali. Utoaji wa vibali ulikuwa holela kiasi kwamba wanasiasa walikuwa ni Miongoni mwa watu waliopewa vibali vya kuagiza sukari wakati wengine hata uwezo wa kuagiza hawana matokeo yake waliwauzia vibali hivyo wafanyabiashara wakubwa walikuja kutengeneza ‘umonopoli’.

3.Udanganyifu. Sukari iliyokuwa inaagizwa nje kuna baadhi ilikuwa haina ubora wa kimatumizi ya binadamu sasa wanachokifanya wafanyabiashara ilikuwa wakiifunga kwenye Mifuko yenye nembo ya viwanda vya ndani.

4.Kutokuwa na sera madhubuti ya kusimamia uagizwaji wa sukari nje ya nchi.

5. Sukari inayozalishwa kwenye baadhi ya viwanda imekuwa inauzwa kwa mtu mmoja tu Ambae alikuwa akifanya mchezo wa kuficha sukari ili bei ipande kutokana uhaba wa sukari kwenye soko kwa makusudi.

6. Sukari imekosa wa kuisemea sababu wanasiasa wengi niwafanyabiashara wa hii bidhaa na Wengine wanavibali vya kuagiza kutoka nje.

No comments:

Post a Comment