Kufanya Vibaya kwa Simba nani alaumiwe?

Na Yahya Njenge
Makocha wengi Duniani wapo kwa ajili ya
kufukuzwa lakini hawafukuzwi wakiwa wamefanya Mazuri bali hufukuza
wakiboronga. Ukiona anaondoka na kafanya makubwa ujue anaenda
kufundisha timu ya taifa ama kapata dili sehemu nyingine. Simba
wamefukuza kocha Anayeitwa Dulan Kerry na kuja Steven Mayanja.
Kery alikuwa mbishi na msimamo wake
ambao ulikuwa na faida kwa soka la bongo kwa Upande mwingine haukuwa na
faida, pamoja na yote yaliyo tokea kwake aliwaunganisha Wachezaji kwa
namna yake alivyoweza kilicho mponza msimamo wake pamoja na udhaifu Mwingine wa kibinadamu. Alichosaidia ni timu kutokuvurugika japo matokeo
hayakuwa Mazuri.
Mayanja amekuja kwa mbwembwe akitokea
Coast Union na mkwara mzito alipata matokeo kwa mechi tano mfululizo,
kwa mara ya kwanza tangu 2013 timu hiyo haukuwahi kufika kileleni mwa
msimamo wa ligi, lakini kwa juhudi na nguvu aliyokuja nayo imeonja japo
kukaa Juu ya ligi kwa siku kadhaa.
Mpira wa Tanzania ukiwa mjuaji sana
unaharibu, alicho kifanya kuleta nidhamu katika timu Ni jambo la msingi
mno lakini sasa limeigharimu timu hiyo. Vijana walikuwa na vipaji vya
hali Ya juu na nia ya kucheza soka. Kessy tayari anaenda Yanga hukumu ya
Banda haijulikani na Isihaka aliko hakujulikani. Mayanja hapaswi
kulaumiwa wachezaji nao pamoja na utoto walipaswa kujiheshimu na kulinda
kibarua chao.
No comments:
Post a Comment