Mrisho Mpoto atasaidia kupunguza maambukizi ya Ukimwi
Kaonga Kasati
Licha ya Kampeni kadhaa kufanywa dhidi ya maambukizi ya UKIMWI nchini Tanzania Ikiwemo ya Tanzania bila ukimwi inawezekana
lakini takwimu za mwisho za mwaka 2015 Chini ya TACAIDS zinaonesha kuwa
maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini yaliongezeka kwenye kundi
la vijana wenye umri wa miaka kati ya 19 mpaka 24 tofauti na
ilivyokuwa miaka mitano iliyopita, ambako kundi lililokuwa limeathiriwa
zaidi lilikuwa miaka kati ya 25 mpaka 34.
Pia licha ya kwamba kiwango cha
maambukizi mapya ya virusi hivyo nchini kimeshuka kutoka asilimia 7
mwaka 2004 mpaka kufikia asilimia 5.3 mwaka jana, takwimu za baadhi ya
mikoa ikiwemo Singida, Kigoma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro na Kagera
zilionekana kuongezeka.
kuendelea kuandamwa na maambukizi hayo,
ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maendeleo na mwingiliano wa
watu, mikoa ya Tanga na Manyara ndiyo yenye takwimu chache za maambukizi
zikiwa na asilimia 4 pekee kwa mwaka 2015.
Huenda kushindwa kufanya vizuri kwa
kampeni zilizopita kulichangiwa na mambo mengi ila kubwa zaidi ni mtu
ambaye anatakiwa kufikisha ujumbe kwenye jamii, Jambo ambalo limeisukuma
Mgodi wa dhahabu wa Geita kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na UKIMWI nchini (TACAIDS) kumteua msanii mashuhuri wa nyimbo za asili nchini Mrisho Mpoto kuwa balozi wa kampeni ya Kili Challenge, ili kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
No comments:
Post a Comment