Na Mwamvita Mtanda
Yanga inaingia katika michuano hiyo hatua ya 16 bora baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2, Aprili 20 mwaka huu.
Esperanca wameingia hatua hiyo baada ya kuwatoa Vita Club Makonda ya Jamhuri ya Congo kwa jumla ya mabao 4-1 katika hatua ya pili ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa Afrika Ngazi ya klabu.
Mara ya mwisho Yanga ilikutana na timu ya Angola mwaka 2007 katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilipocheza na Altetico Petroleos Luanda na kuitoa katika raundi ya kwanza kwa jumla Ya mabao 3-2 baada ya ushindi wa 3-0 nyumbani na kufungwa 2-0 katika mechi ya marudiano wakiwa ugenini.
Yanga chini ya kocha wake Hans van de Pluijm, inaingia uwanjani ikiwakosa wachezaji wake Wawili tegemeo, mshambuliaji Donald Ngoma na kiungo Thaban Kamusoko wanaotumikia Adhabu ya kadi mbili za njano.
Wakati nafasi ya Ngoma ikitarajia kuzibwa na Haruna Niyonzima na Salum Telela, upande wa Kamusoko kunaonekana kuna kazi kubwa.
Mchezo huo utachezeshwa na Joseph Odartei Lamptey atakayepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera David Laryea na Malik Alidu Salifu wote kutoka Ghana, wakati kamisaa ni Asfaw Luleseged Begashaw kutoka Ethiopia.
Timu hizo zinatarajia kucheza mechi ya marudiano baada ya wiki mbili nchini Angola.
Iwapo Yanga itafanikiwa kuishinda Sagrada Esperanca baada ya michezo yote miwili itaingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Wakati huo huo, uongozi wa Yanga umetangaza viingilio katika mchezo huo utakaoanza saa 10:00 jioni ambapo Jukwaa la VIP A ni Sh 30,000, VIP B na C Sh 20,000, jukwaa la viti vya Rangi ya chungwa Sh 7,000 na mzunguko wa viti vya bluu na kijani Sh 5,000.
No comments:
Post a Comment