Friday, 6 May 2016

Simba yapigwa faini na Fifa kupuuza kumlipa Mchezaji Donald Musoti Raia wa Kenya


images 
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba Baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo Ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo.

Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.

Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa Alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa Na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika Usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.

Felix Majani, Mwanasheria wa Musoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA, Alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.

Kwa kosa hilo Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 kuanzia Tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016. TFF imekuwa nakala na maagizo kuisimamia Simba inalipa kiasi hicho cha fedha.

Simba imeagizwa kulipa stahiki zote za Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea Barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016.

Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha inalipa Na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi zake Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara –VPL.

FIFA imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo kama haitalipa katika muda Uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, FIFA itaishusha Simba daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.

Kwa upande wake, TFF imagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji Wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment