Mamlaka
ya Mapato Tanzania TRA imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5319 yenye
thamani ya Zaidi ya Shilingi Million 373.5 kwa Taasisi mbali mbali
Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA
kuwa ni Salama kwa matumizi.
Sukari
hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani
ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini
Brazil kupitia Zanzibar.
Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Million 246.
No comments:
Post a Comment