Friday, 6 May 2016

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato TRA Alphayo Kidata Wamekusanya Shilingi Trilioni 10.9 Mwaka wa Fedha 2016/2017


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezidi kuvuka malengo ya ukusanyaji Mapato kwa kukusanya asilimia 99 ya lengo la kukusanya mapato kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kukusanya Shillingi Trillioni 10.9 kutoka katika lengo la Trillion 11.

Akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa makusanyo Ya mapato nchini leo  Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema wanaendelea na jitihada Mbalimbali kuhakikisha wanafikia na kuvuka lengo la makusanyo kwa Mwaka wa fedha 2015/2016 licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali Zinazowakabili.

“Kwa kipindi cha miezi miwili iliyobaki kabla ya mwaka wa fedha mpya kuanza tumedhamilia kukusanya zaidi ya Shillingi Trillioni 1.4 ili kufikia na kuvuka lengo la mwaka wa fedha 2015/2016 tulilowekewa.”Alisema Kidata.

Kamishna Alphayo Kidata ameongeza kuwa wanaendelea kudhibiti wafanyabishara wanaokwepa kodi kwa kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo kutumia mashine za kieletroniki za EFD’s ili kuiwezesha mamlaka Hiyo kukusanya mapato kwa urahisi na kufikia malengo waliyowekewa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato ili kuweza kufikia au kuvuka malengo kwa mwaka huu wa Fedha ikiwemo kuendelea kupambana na magendo, kuziba mianya ya Upotevu wa mapato na kusimamia mifumo ambayo inamrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu wowote.

No comments:

Post a Comment