
Kesi inayomkabili malkia wa China, Yang Feng Glan (66) Malkia wa Meno ya Tembo na wenzake, imeahirishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Kisutu jijini hapa, leo Januari 3, 2017 kutokana na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kutokuwepo mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa kuwa yupo likizo.
Aidha watuhumiwa wamerudishwa rumande na kuamuriwa kurudi tena mahakamani hapo mnamo Januari 16, mwaka huu kwa ajili ya kupangiwa siku nyingine ya kusikiliza kesi yao.
Glan maarufu kwa jina la Malkia wa Meno ya Tembo anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara Salvius Matembo (39) na Manase Philemon (39).
Baada ya hati kuwasilishwa, washtakiwa walisomewa mashtaka ambayo waliyakana. Upande wa mashtaka ulidai upelelezi umekamilika. Wanadaiwa kati ya Januari Mosi 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za Serikali bila kibali.
Katika kipindi hicho wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 zenye thamani ya Sh5.4 bilioni bila leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.
No comments:
Post a Comment