Mkurugenzi wa
Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Agness
Mtawa akikabidhi vitanda vitano kwa Mganga Fawidhi wa Hospitali ya
Wilaya ya Mafia, Abdallah Bhai. Vitanda hivyo vimetatumika kwa kina mama
wakati wa kujifungua.
Mkurugenzi wa
Huduma za Uuguzi na Ukunga wa hospitali hiyo, Bi. Agness Mtawa
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vitanda hivyo.
Mganga
Fawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia, Abdallah Bhai akizungumza na
waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Dar essalaam,
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imetoa msaada wa vitanda 20 vinavyotumika wakati kina mama wanapojifungua kwa Hospitali ya Wilaya ya Mafya , Hospitali ya Sinza-Palestina pamoja na Hospitali ya Temeke.
Kati
ya vitanda hivyo , Hospitali ya Temeke watapatiwa vitanda vinane,
Hospitali ya Sinza -Palestina vitanda saba wakati Hospitali ya Wilaya ya
Mafya wamekabidhiwa vitanda vitano leo.
Akikabidhi
msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili , Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa amesema lengo ni kuboresha huduma za afya na kumuwezesha mama kujifungua katika mazingira salama.
“Tulipata
taarifa kwamba wenzetu wanahuitaji mkubwa wa vitanda vya kujifungulia
hivyo tukaona tuwasaidie na hatutaishia hapa tutaendelea kushirikiana
kadiri inavyowezekana,” amesema Sister Mtawa.
Akipokea
msaada huo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafya, Abdalah
Bhai amesema msaada huo umekuja wakati muafaka na kwamba vitanda hivyo vitakidhi mahitaji.
“
Hospitali ya Wilaya ya Mafya ilikua inahitaji vitanda vitano vya
kujifungulia na leo wenzetu Muhimbili wametupatia vitanda hivyo, hivyo
kulingana na mahitaji yetu tunawashukuru sana, tunawaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia vitendea kazi vingine,” amesema Mganga Mfawidhi Bhai.
Kwa mujibu wa Mganga huyo Mfawidhi awali hospitali hiyo ilikuwa na vitanda vya kujifungulia vitatu ambavyo vipo chini ya kiwango.
No comments:
Post a Comment