
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu ametuma timu ya Maofisa wa Polisi ikiongozwa na
Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa kwenda Zanzibar kushughulikia
kero na malalamiko ya wananchi juu ya vitendo vya udhalilishaji na
ukatili kwa watoto/wanawake ambavyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.
Timu hiyo imepewa jukumu la
kuchunguza vitendo hivyo vya udhalilishaji na kiini chake na hatimaye
kuja na mpango mkakati wa kuzuia vitendo hivyo ikiwemo kuwakamata
wahusika na kuwafikisha mahakamani.
IGP Mangu amewataka wananchi wa
Zanzibar, Taasisi za kiserikali na Taasisi za kiraia zilizopo Zanzibar
kutoa ushirikiano kwa timu hiyo ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni
kinyume na maadili ya Watanzania.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment