Wednesday, 18 January 2017

Mawaziri wazidi kujiuzulu Gambia

Mawaziri wazidi kujiuzulu GambiaMawaziri watatu nchini Gambia wamejiuzulu wakati Rais Yahya Jammeh akipuuza wito wa kumtaka aondoke madarakani wakati muhula wake utakapokamilika siku ya Alhamisi.
Yahya Jammeh aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1994.

Baada ya uchaguzi mkuu kufanyika Adama Barrow alimshinda Yahya Jammeh na mwanzoni Yahya alikubali matokeo haya lakini ghafla baada ya siku chache alipinga matokeo hayo na kusema kuwa yana hitilafu.
Kwa mujibu wa habari wiki iliyopita waziri wa habari Sheriff Bojang na waziri wa michezo Alieu Jammeh nao walijiuzulu.
Na sasa mawaziri wa mashauri ya nchi ya kigeni,fedha na biashara wametangaza kujiuzulu.
Hata hivyo mpaka sasa maelfu ya wananchi wamekuwa wakikimbilia nchi za jirani na Guinea-Bissau kwa hofu ya kutokea kwa ghasia siku za usoni.

No comments:

Post a Comment