Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu
Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akifungua semina ya mafunzo ya
haki za wanawake wanaoshiriki katika mradi huo iliyofanyika mwishoni
mkwa wiki Kinondoni jijini Dar es salaam.
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu
Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akimtambulisha WIGAYI
KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC)
mkufunzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam.
WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akitoa mafunzo katika semina hiyo.
WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo
cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akifafanua jambo wakati
alipokuwa akitoa mafunzo katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu
Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) na Victor Francis-Meneja Mafunzo
wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) wakiwa katika semina hiyo.
Wanawake wanaoshiriki katika
mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) unaoendeshwa na Kampuni ya AFREXA
International Ltd, wametakiwa kufahamu haki mbalimbali za binadamu
zinamwongoza mwanadamu kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo.
Akizungumza Jijini DSM, wakati wa
semina ya siku moja ya wanawake kuelekea katika mafunzo ya kuendesha
vyombo vya moto vya biashara, mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa
Sheria kwa Wanawake (WLAC) WIGAYI KISSANDU amesema ni muhimu kwa
wanawake kufahamu haki hizo kwa kuwa zinatoa mwongozo kufikia malengo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) MARTIN GABONE amesema semina hiyo
ni moja ya hatua za mwanzo za mafunzo ya udereva kwa wanawake kwa ajili
ya kuendesha vyombo vya moto vya biashara na kusisitiza wanawa wajibu
wa kuhakikisha wanawake hao wanaingia rasmi katika sekta ya usafirishaji
kwa kuajiriwa au kujiajiri.
Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani
(WOW) hadi sasa umesajili zaidi ya wanawake 200 kutoka maeneo
mbalimbali nchini, ili waweze kuwapatia bure mafunzo ya udereva wa
vyombo vya moto vya biashara ambapo baada ya mafunzo hayo watatafutiwa
ajira na wengine watawezeshwa ili waweze kujiajiri.
No comments:
Post a Comment