Friday 13 May 2016

Waamuzi kutoka Tanzania kuchezesha kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana

 

 

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limewateua waamuzi wanne kuchezesha mchezo Na. 27 kati ya Ethiopia dhidi ya Ghana kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana 2017. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Addis Ababa (Gazon Nature), jijini Addis Ababa huko Ethiopia.

Mchezo huo utachezwa Mei 22, 2016 majira ya saa 10.00 jioni kwa saa za Ethiopia, utaamualiwa na Mfaume Ali Nassoro atasimama katikati wakati walioteuliwa kuwa waamuzi wa pembeni ni Josephat Deu Bulali (line 1) na Alli Kinduli na mezani atakuwa Martin Eliphas Sanya.

Kamishina wa mchezo huo kwa mujibu wa CAF ni Julius Elly Mukolwe kutoka Kenya.

No comments:

Post a Comment