Mwili
wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki
ukiwasili kwa hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya
Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais
Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa
Kenya Mh.Mwai Kibaki kufuatia kufiwa na mke wake mpendwa Mama Lucy
Kibaki mjini Nairobi,nchini Kenya anaeshuhudia kulia ni Rais wa
Kenya,Uhuru Kenyatta.
Naibu
Rais wa Kenya Mh.William Rutto na Mkewe wakimfariji Rais Mstaafu wa
Kenya Mh.Mwai Kibaki wakati wa mazishi ya Mkewe Lucy Kibaki
yaliyofanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini
Nairobi nchini Kenya,Pichani shoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akishuhudia tukio
hilo.
Rais
wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu
ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete wakati wa
mazishi ya Mama Lucy Kibaki hapo jana mjini Nairobi,kulia ni mke wa Rais
Uhuru Kenyatta,Bi Margaret Kenyatta.
Rais
Mstaafu wa Kenya,Mh.Mwai Kibaki akiweka udogo kwenye kaburi la Mke wake
Mama Lucy Kibaki,wakati wa mazishi yaliyofanyika hapo jana katika eneo
la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka
udogo kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama
Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la
Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka
shada la maua kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai
kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la
Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,ambapo nchini
Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Rais
Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete Amekuwa
miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika
Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la
Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.
Marehemu
Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea Mazingira
safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na
wema katika familia.
Kikwete
ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha
mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika
katika ukanda wa Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment