Thursday 16 November 2017

Sayari mpya yagundulika


Wataalamu wa anga za juu wamegundua sayari isiyo na joto sana na yenye ukubwa unaokaribia sana na wa dunia.
Sayari hiyo inapatikana karibu na mfumo wetu wa Jua
Mandhari katika sayari hiyo ambayo imepewa jina Ross 128 b yanaifanya kuwa pahala pazuri pa kutafuta viumbe au uhai anga za juu.
Sayari hiyo inapatikana umbali wa miaka 11 kwa kasi ya miali ya jua, na ndiyo sayari ya pili kwa karibu zaidi ambayo ina mazingira yanayokaribiana na ya dunia.
Sayari ya aina hiyo iliyo karibu zaidi hufahamika kama Proxima b, na wataalamu wanasema mazingira huko hayaonekani kuwa mazuri sana kiasi cha kuweza kuwa na viumbe.
Proxima b iligunduliwa 2016, na huzunguka kwenye mzingo ulio kwenye nyota kwa jina Proxima Centauri, ambayo hufahamika kama "nyota nyekundu mbilikimo". Nyota hiyo huwaka sana na ina maana kwamba milipuko kwenye nyota hiyo huenda ikarusha miali nururishi yenye sumu kwenye sayari ya Proxima b.
Sayari hiyo mpya, Ross 128 b, huzunguka sayari ambayo haitofautiani sana na Proxima Centauri (pia ni nyota nyekundu mbilikimo), lakini hailipuki sana.


  • Mpango wa Marekani kupeleka watu Mars

  • Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars

  • Sababu ya chombo cha Ulaya kutoweka Mars
Mmoja wa waliogundua Nicola Astudillo-Defru kutoka kituo cha kutazama anga za juu chenye makao yake Geneva, Uswizi aliambia BBC kwamba kwa sababu Proxima Centauri hulipuka na kutoa miali nururishi yenye sumu, "nafikiri ndio, Ross 128 ni pahala pazuri zaidi pa uhai kunawiri."
"Lakini bado hatufahamu anga ya Ross 128 b iko vipi. Kwa kutegemea vitu vilivyo kwenye anga yake na uwezo wa mawingu kuakisi mwanga, huenda kukawa na maji ambayo yanaweza kufanikisha uhai kama hapa duniani, au iwe sayari kama vile Zuhura ambayo haiwezi kufanikisha uhai."



Sayari hiyo mpya iligunduliwa na darubini yenye uwezo mkubwa kwa jina Harps iliyopo katika kituo cha kufuatilia anga za juu cha La Silla nchini Chile.



Ingawa kwa sasa sayari hiyo ipo miaka 11 kwa kasi ya miali ya jua kutoka kwenye dunia, nyota asili Ross 128 inasonga kuelekea kwa dunia na huenda ikaipita Proxima Centauri na kuwa mfumo wa nyota ulio karibu na dunia zaidi katika kipindi cha miaka 79,000.

  • Proxima Centauri ni 'nyota nyekundu mbilikimo'; ni ndogo na pia haina joto sana kama Jua

  • Inakaribia zaidi lakini kuna uwezekano ikawa imeunganishwa kwa mvuto na Alpha Centauri A & B

  • Kwa mtu anayetumia jicho lake kutazama juu angani Alpha Centauri A & B huonekana kama nyota moja

  • Sirius A ndiyo nyota inayong'aa zaidi na inayotambulika kwa urahisi zaidi angani usiku

  • Jupiter ndiyo sayari kubwa zaidi mfumo wetu wa Jua. Iwapo ingelikuwa na uzito mara 80 zaidi ya sasa, basi ingegeuka na kuwa jua
  • Mambo muhimu kuhusu sayari ya Mars

  • Mmarekani wa kwanza kuizunguka dunia afariki

  • Japan yatuma mtambo wa kufagia anga za juu


No comments:

Post a Comment