Tuesday 14 November 2017

Takukuru yatangaza donge nono kwa atakayetoa taarifa za Gugai alipo

TAKUKURU wanamtafuta Godfrey John Gugai kwa kuwa na maisha na mali yanayozidi kipato chake bila maelezo
Huyu alikuwa mtumishi wa umma TAKAKURU na ameweza kujiptia mali nyingi, mwazoni TAKUKURU walimwita na kumhoji lakini baadae alipoona anakosa maelezo alikuwa anawapiga chenga na kukimbia nchi kupitia njia zisizo rasmi
Mpaka sasa anatafutwa bado hajaapatikana na wametangaza kwa mwananchi yoyote atakayempata atoe taarifa
TAKUKURU watatoa zawadi ya milioni 10 kwa ambaye atafanikiwa kupatikana kwa bwana huyo
Ametaja mali anazomiliki mtu huyo ikiwa ni pamoja na jengo la ghorofa nne lililopo Ununio Kinondoni, Jengo la Kifahari la ghorofa tatu
Ana nyumba za kupangisha Kinondoni, jengo la kifahari lililopo Majita Musoma, Jengo la Kifahari Kiseke Mwanza, Jengo la Kifahari Nyegezi Mwanza

Pia anailiki viwanja maeneo ya Bunju Kinondoni, Kigamboni, Buyuni Temeke, viwanja viwili Kaole Bagamoyo, Kibaha, Kihonda Morogoro, Kiyeheya Morogoro, Lukuvi Morogoro, Kisasa Dodoma, Itege Dodoma, Chidati Ngolo Mwanza, Mgongolo Mwanza, Nyamagana Mwanza, Nyamagana Mwanza, Magarika Mwanza, Makoko Musoma, Gomba Arusha, viwanja 3 Mwambani Tanga, Viwanja 2 Mwakidila tanga, gari aina ya Mitsubishi Canter, Toyota Rav 4,na pikipiki ,

No comments:

Post a Comment