Wednesday 15 November 2017

Nyalandu apata vitisho vingi

Image result for nyalandu
Ndg, Lazaro Nyalandu na Familia yake
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini. Mh. Lazaro Nyalandu ameomba kuombewa yeye pamoja na familia yake kwa kudai kwamba  amekuwa akipokea vitisho visivyo na idadi baada ya kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Usiku wa kuamkia leo Nyalandu ametumia ukurasa wake wa twittter ambao ameonyesha hofu yake na kudai kwamba njia zote zinatumika kuhakikisha ananyamazishwa.
"Napokea  idadi isiyo ya kawaida ya vitisho tangu kuondoka CCM chama cha tawala. Ni ajabu kuwa kuna hofu kubwa kutoka kwa wasomi, ambao wanatumia njia zote zinazowezekana kuninyamazisha" Nyalandu
Ameongeza "Tafadhali niombeeni mimi pamoja na familia yangu wakati wa majaribu haya tunayopitia".

Kabla ya kuhamia Chadema mapema mwanzoni mwa mwaka huu, Nyalandu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM.

No comments:

Post a Comment