Wednesday 29 November 2017

Sasii kuchezesha michuano ya Kombe la CECAFA Challenge


Waamuzi wawili wa soka nchini wameteuliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ajili kuchezesha michuano ya Kombe la CECAFA Challenge itakayofanyika nchini Kenya.

CECAFA imewataja mwamuzi wa kati Elly Sasii na mshika kibendera Soud Lila, kutoka Dar es Salaam kuwa sehemu ya waamuzi wa michuano ya CECAFA 2017.
Mbali na waamuzi hao, CECAFA pia imewateua kocha Sunday Kayuni ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na Mjumbe Mteule wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Iddi Mgoyi kuwa wajumbe wa Kamati ya Maandalizi.
Waamuzi hao wawili na wajumbe wawili wanatarajiwa kusafiri kwenda nchini Kenya Novemba 30 mwaka huu, tayari kwa kushiriki taratibu nzima za maandalizi hayo ambapo michuano itaanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu.

Timu ya taifa ya Tanzania Bara Kilimanajaro Stars na ile ya Tanzania Visiwani Zanzibar Heroes zipo kwenye maandalizi ya michuano hiyo. Timu hizo zimepangwa kundi moja sambamba na timu za Libya na Rwanda.

No comments:

Post a Comment