Sunday 26 November 2017

Mawakala wa vyama wapata wakati mgumu

 Mawakala wa vyama vya CCM, Chadema na ACT Wazalendo kwenye Kata ya Makiba wilayani Arumeru wamezuiwa kuingia katika vyumba vya uchaguzi kwa madai ya kukosa vibali.
Kata hiyo ina jumla ya vituo 14 na hadi hivi sasa upigaji kura unaendelea bila kuwepo kwa mawakala hao 42 wa vyama hivyo.
Mgombea udiwani wa CCM katika kata hiyo Samson Laizer  Leo Jumapili kuwa mawakala wake kuzuiwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura.
Vilevile wakala wa Chadema wa Kituo cha Kanisani A,  Adam Woisso amesema japokuwa alikuwa na barua ya utambulisho wa chama hicho na barua ya uthibitisho ya Tume ya Taifa ya  Uchaguzi(NEC) lakini alizuiwa kuingia ndani.
Kwa upande wake wakala wa ACT Wazalendo, Said Yusuf amesema alizuiwa kuingia kwa sababu ya kukosa barua kutoka NEC.
Mgombea udiwani wa ACT Wazalendo, Ernest Maturo amesema hizo ni mbinu za kuhakikisha mgombea udiwani anayetakiwa kushinda na tume anashinda nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment