Monday 27 November 2017

Meya Boniface wa Ubungo apata Dhamana

 Image result for boniface jacob
Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa polisi kwa takriban saa 15 akidaiwa kutaka kupanga njama za vurugu baada ya matokeo ya udiwani wa Kata ya Saranga kutangazwa.
Jacob ambaye pia ni diwani wa Ubungo (Chadema) alikamatwa na polisi jana Jumapili Novemba 26,2017 saa tano asubuhi katika kituo cha kupigia kura cha Mtakatifu Peter, Kimara.

Akizungumza leo Jumatatu Novemba 27,2017 baada ya kuachiwa na polisi, Jacob amesema alipokamatwa alipelekwa vituo vya Mbezi kwa Yusuf, Mabatini na baadaye Oysterbay alikokaa muda mrefu.

"Nimeachiwa saa 7:40 usiku kwa dhamana, hizi zote zilikuwa ni njama za kutunyima ushindi. Dhamana gani inatolewa usiku?” amehoji Jacob.

Amesema, "Hii ilikuwa mipango ili Chadema isishinde ila wakazi wa Ubungo wasivunjike moyo na haya, wamejionea hali halisi iliyofanyika na huu ni ushindi kwetu."


Jacob ambaye  pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema ametakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay leo.

No comments:

Post a Comment