Saturday 18 November 2017

Maafisa wanne wa polisi kuchukuliwa hatua kwa mauaji ya mtoto wa miezi 6

Maafisa wanne wa juu huko Kisumu Kenya wanatarajiwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mauaji ya mtoto wa miezi 6 Samantha Pendo kilichotokea wakati wa vurugu za uchaguzi mwezi wa nane
Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Keriako Tobiko ameagiza Jeshi la polisi kuwachukulia hatua maafisa waandamizi na pia kuagiza uchunguzi wa wa Stephanie Moraa Gisemba mwenye umri wa miaka 8 huko Nairob
i uanze
Jeshi la polisi pia litatakiwa kuwalipa fidia familia zilizoathirika
Watoto hao waliuawa na polisi waliokuwa wameagizwa kuzuia maandamano huko Mathare na Nyalenda
Hii inakuja siku chache baada ya Mamlaka Huru ya Kuchunguza Utendaji wa Polisi kutangaza kuwa imekamilisha uchunguzi juu ya mauaji 12 yaliyofanywa na polisi na kupeleka mafaili yake kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali

No comments:

Post a Comment