Thursday 16 November 2017

TFF kuwachulia hatua waliosambaza ujumbe wa kuongeza posho kwa wajumbe

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao ametolea ufafanuzi ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ukiituhumu taasisi hiyo inayoongoza soka la Tanzania kuongeza posho kwa wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na kuanzisha malipo ya mishahara kwa Rais na makamu wake.

1. Viwango vya posho za vikao vya Kamati ya Utendaji havijawahi kujadiliwa wala kubadilishwa (kuongezwa). Bado vipo vilevile.
2. Wajumbe wa kamati ya utendaji wanawezeshwa kutekeleza majukumu yao kwenye kanda zao. Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni kazi ya kujitolea watakuwa wakipewa Tsh. 1.5 milioni kwa miezi mitatu kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao kwenye Kanda zao (Tsh. 1.5 milioni ni sawa na Tsh. 500,000 kwa mwezi).
3. Kuhusu mshahara wa Rais wa TFF na makamu wake jambo hilo halikufikiwa mwafaka na Kamati ya utendaji. Wajumbe wa kamati ya Utendaji walishauri ofisi ya Rais ihudumiwe na TFF kama ilivyo kwa ofisi za marais wa FIFA na CAF.
Rais wa TFF Wallace Karia alikataa kwa kusema, anaamini sio wakati mwafaka wa yeye kuchukua posho hadi taasisi itakapokaa vizuri na taratibu zote kufuatwa.
Hatua zilizochukuliwa
Kidao amwagiza mwanasheria wa TFF kufungua mashtaka (leo) kwa wale waliosambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wenye lengo la kuichafua taasisi hiyo.

No comments:

Post a Comment