Miongoni mwa mitumbwi iliyokuwa
imezagaa katika mwambao wa ziwa Tanganhyika Kijiji cha Wampembe ambayo
mingi haikuwa na usajili na kuipotezea serikali mapato katika sekta ya
uvuvi.
Mmoja wa maafisa wa Sumatra
(mwenye overoli la bluu) akitoa ufafanuzi mbele ya Mh. Zelote (mwenye
kaunda suti0 pamoja na maafisa mbalimbali walioambatana katika ziara
hiyo kwenye kijiji cha Wampembe, Wilayani Nkasi.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa kamishna
Mstaafu zelote Stephen (kushoto) akimuonesha Afisa Uvuvi wa Kata Godfrey
kashengebi (kulia) nyavu zilizobainika kutokidhi vipimo vilivyokubalika
na serikali katika shughuli za uvuvi na kuagiza kukamatwa kwa kokoro
hizo zilizokuwa zikiendela kutumiaka bila ya kukaguliwa na afisa huyo.
vijana wakiwa wamebeba kokoro zilizoagizwa kukamatwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa na kufikishwa ofisi ya kata.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna
Mstaafu Zelote Stephen ametoa siku saba kwa Halmashauri ya Wilaya ya
Nkasi, Kalambo pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu na
majini (SUMATRA) kumpatia orodha kamili ya vyombo vyote vya majini
vinavyofanya shughuli zake katika mwambao wa ziwa Tanganyika katika
Wilaya za Nkasi na Kalmbo za Mkoa wa Rukwa.
Ametoa agizo hilo alipotembelea
mwambao wa Ziwa Tanganyika katika Kijiji cha Wampembe, Kata ya Wampembe
Wilaya ya Nkasi na kubaini mitumbwi kadhaa iliyokuwa ikizagaa kwenye
mwambao huo ikiwa haijafanyiwa usajili na kusababisha upotevu wa mapato
ya serikali kupitia sekta hiyo ya uvuvi.
“Halmashauri zimekuwa zikilalamika
hazina mapato ya kutosha wakati naona pesa zikielea tu hapa na Hakuna
chochote kinachoendelea, sasa natoa siku saba kwa Halmashauri na SUMATRA
nipate orodha kamili ya vyombo vyote vya usafiri wa majini, usajili wao
na leseni zao zinazowaruhusu kufanya shughuli za uvuvi katika mwambao
huo.” Amesema.
Pamoja na hayo agizo hilo pia
limekuja baada ya wiki moja iliyopita boti ambayo mmiliki wake
hakujulikani kuzama ziwa Tanganyika ikitokea katika Kijiji cha Kalila,
Kata ya kabwe, tarafa ya Kirando, Wilayani Nkasi kuelekea Kijiji cha
Kyala Mkoani Kigoma na kupelekea kifo cha mtoto mmoja na watoto wengine
wawili kuhofiwa kufa maji huku watu 11 wakiokolewa. Na wafanyakazi
wawili wa boti hiyo kukimbia.
Katika kuhakikisha usalama wa
Kijiji cha Wampembe unaimarika Mh. Zelote aliagiza kuhamishwa kwa
watumishi wawili, Afisa Mtendaji wa kata ya Wampembe Faustine
Wakulichamba pamoja na Afisa uvuvi wa Kata Godfrey Kashengebi kwa makosa
mbalimbali moja ikiwa kutosimamia makusanyo ya mapato ya uvuvi jambo
lililopelekea kudorora kwa makusanyo ya mapato pamoja na kuwepo kwenye
kata hiyo kwa miaka zaidi ya sita jambo ambalo linapunguza ufanisi wao
wa kazi.
Katika doria hiyo Mh. Zelote pia
alikamata kokoro na nyavu kadhaa zilizokuwa hazikukidhi vipimo vya
serikali katika matumizi yake jambo ambalo maafisa hao walifumbia macho
na kuisababishia serikali upotevu wa mapato.
Kwa mujibu wa sheria za halmashauri mtumbwi wenye urefu wa mita 4 hulipiwa dola 4 kwa mwaka kama ada ya usajili.
No comments:
Post a Comment