Timu ya Manchester United imezidi
kujiweka katika nafasi nzuri ya kutafuta ubingwa wa Ligi Kuu ya England
baada ya kupata ushindi mnono wa jumla ya magoli 4-0 dhidi ya Vibonde
Crystal Palace mchezo uliopigwa kwenye dimba la Old Traford.
Magoli ya Man United yakifungwa na Fellaini aliyefunga mawili dakika ya 35 na 49,Juan Mata dk 3 na Lukaku 86.
Kwa Matokeo hayo Man United wanabaki
kwenye nafasi yao ya pili wakiwa na alama 19 sawa na Man City wakiwa
wanatofautiana magoli ya kushinda na kufungwa Vijana wa Mourinho
wamefunga magoli 21 na kufungwa mawili huku Guardiola akiwa ameshinda
magoli 22 na kufungwa mawili.
MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia
7, Jones 7, Smalling 6.5, Young 7; Matic 6, Fellaini 8; Mata 7.5
(Herrera 76 mins, 6), Mkhitaryan 5.5 (Lingard 66, 6), Rashford 7
(Martial 71, 7); Lukaku 6
Subs not used: Bailly, Blind, Romero, Darmian
Goals: Mata 3mins; Fellaini 35, 49; Lukaku 86
CRYSTAL PALACE (4-3-3): Hennessey 6; Ward 5.5,
Sakho 6, Delaney 5.5, van Aanholt 6; Townsend 6, Milivojevic 6, Puncheon
5.5 (Riedewald 69, 5.5); Cabaye 6.5, Sako 6.5 (Ladapo 74), Schlupp 5.5
(McArthur 69, 6)
Subs not used: Speroni, Lee, Mutch, Kelly
Referee: Mike Dean 6
Attendance: 75,118
Katika uwanja wa
Darajani wenyeji Chelsea wamepoteza mechi yao baada ya kufungwa goli 1-0
na Manchester City huku Chelesea wakipata pigo kutokana mshambuliaji
wao Moratta kupata majeraha.
Goli la ushindi la Man
City limefungwa na Kevin De Bruyne kipindi cha pili kwa shuti kali na
kumshinda mlinda mlango dakika ya 67 Courtois
No comments:
Post a Comment