Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha ofisini
kwake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird ambaye alimtembelea Makamu
wa Rais ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird mara
baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Picha na Makamu wa Rais
Makamu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo
amkutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
nchini Bi. Bella Bird, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais na Mkurugenzi huyo walizungumzia masuala mbalimbali ya Lishe kwa
akina Mama na namna ukosefu wa lishe bora unavyopelekea vifo vya akina
mama na watoto wakati na baada ya kujifungua.
Aidha wamesisitiza suala la Elimu ya Lishe Bora kwa wakina mama hao ili kukabiliana na tatizo.
Makamu wa
Rais aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuwasaidia wakina mama wa
Kitanzania na kuitaka iendelee kufanya hivyo hasa wakati huu ambapo nchi
inaenda kwenye uchumi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment