Wednesday, 20 September 2017

Iran yapuuzia hotuba ya Trump, UN

Iran imeipuuzia hotuba ya kwanza ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyoitoa katika Umoja wa Mataifa mjini New york na kuiita kuwa ni hotuba yenye chuki ya kijinga.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif katika mtandao wake wa Twitter ameiita hotuba hiyo ya Rais Trump kuwa ni ya zama za kati.
Rais wa Marekani ameituhumu serikali ya Iran kwamba ni utawala wa kiuaji na kupendekeza kuwa hata yaheshimu makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa chini ya uongozi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Barack Obama.
Rais Trump alitishia pia kuiteketeza Korea kaskazini iwapo shughuli zake za kinyuklia zitaihatarisha Marekani au washirika wake.

Rais huyo wa Marekani katika hotuba yake hiyo ya Umoja wa Mataifa hakuacha pia kuitaja Venezuela.

No comments:

Post a Comment