Mwakilishi wa Shirika la Afya
Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael akizungumza na washiriki
wa mkutano wa mwisho wa Jumuia ya nchi za Afrika, Caribean na Pacific
(ACP) wa kumiarisha mifumo ya kifamasia unaofanyika Hoteli ya Zanzibar
Beach Resort Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya
Duniani (WHO) Dkt. Suzanne Hill akitoa hotuba katika ufunguzi wa mkutano
wa mwisho wa kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa dawa kwa nchi za ACP
katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Wajumbe wa mkutano wa mwisho wa
kuimarisha mifumo ya kifamasia wan chi za kanda ya Afrika Caribean na
Pacific wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika Hoteli ya
Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
nchi za ACP Balozi Emile Ognimba akizungumza na washirki wa mkutano wa
mwisho wa kuimarisha mifumo ya kifamasia unaofanyika Zanzibar Beach
Resort Mbweni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Zanzibar Bi. Asha Abdalla Ali akifungua mkutano wa mwisho wa kuimarisha
mifumo ya kifamasia unaoshirikisha mataifa ya Afrika Caribean na Pacific
katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.
Picha na MAKAME MSHENGA.
Na Ramadhani Ali – Maelezo
Tanzania imefaidika na imepiga
hatua kubwa katika kufuata sheria na kuboresha uingizaji wa dawa na
vifaa tiba sahihi kufuatia msaada mkubwa wa Jumuia ya nchi za Afrika,
Caribean na Pacific (ACP) katika kudhibiti mifumo ya kifamasia kwa nchi
za ukanda huo.
Akifungua mkutano wa mwisho wa
Jumuiya ya nchi za ACP inayofadhiliwa na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya,
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Ali alisema
imefanikiwa kupanga mikakati kuhakikisha dawa zote zinazoingia nchini ni
salama kwa matumizi ya binadamu.
Alisema Jumuiya imewajengea uwezo
wafamasia kwa mafunzo mbali mbali ya kuboresha upatikanaji, usambazaji
na kusajili dawa zinazoingia ili kuhakikisha zilizokuwa chini ya
kiwango haziingizwi nchini.
Katibu Mkuu aliongeza kusema kuwa
Jumuiya ya nchi za Ukanda wa Afrika, Carbean na Pacific imefanya juhudi
ya kuimarisha Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar na kuhakikisha
inatekelezaji majukumu yake kwa ufanisi.
Aidha aligusia kuwa Jumuiya
imeiwezesha Serikali kufanya mapitio ya sera yake ya dawa ili kuona
inaendana na wakati wa sasa kwa mujibu wa mahitaji na kuimarisha afya
za wananchi.
Bi. Asha alilishukuru Shirika la
Afya Duniani na Jumuiya ya nchi za ukanda wa Afrika, Caribean na Pacific
kwa misaada yao mikuwa katika kuimarisha mifumo ya ufamasia nchini.
Akiwakaribisha wajumbe wa mkutano
huo kwa niaba ya mwakilishi wa Shirikala Afya Duniani nchini Tanzania,
mwakilishi wa Shirika hilo Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael alisema
jukumu la kuwa na dawa salama katika nchi linahitaji mashirikiano ya
wadau mbali mbali ikiwemo taasisi za serikali, viwanda vya uzalishaji na
waingizaji dawa.
Akizungumza katika mkutano huo,
Mfamasia Mkuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania Hendry Kigunde alisema
Jumuiya imetoa msukumo mkubwa katika kipindi cha miaka mitano tokea
ilipoanzishwa kwa kuimarisha usambazaji wa dawa kwa njia za kisasa.
Alisema Serikali imefanikiwa
kuboresha miongozo ya uingizwaji wa dawa na kuoredhesha dawa muhimu
ambazo waingizaji wanashauriwa kuzipa kipaumbele kwa ajili ya matimizi
ya wananchi.
Mkutano huo wa siku mbili utafanya
mapitio katika kipindi cha miaka mitano cha Jumuiya ili kujua
mafanikio yaliyopatika katika kutandika mifumo sahihi ya dawa kwa nchi
wanachama na kufahamu changamoto zilizojitokeza katika kipindi
hicho.
No comments:
Post a Comment