Mugabe ameongea hayo Jumatano ya wiki iliyopita baada ya kurejea nchini Zimbabwe akitokea Marekani kwenye mkutano wa umoja wa Mataifa ambako Rais Trump alitamka kuwa endapo atapata ruhusa ya kuishambulia Korea Kaskazini basi ataiangamiza kwa muda mfupi.
Mugabe amesema kwa sasa kila nchi inauwezo wa kumiliki silaha za nyuklia na sio kwa nchi kubwa hiyo dhana imekufa huku akihimiza kila taifa lijitegemee kiutawala pasi kuingiliana.
“Hakuna nchi inayoruhusiwa kuipelekesha nchi nyingine kwenye masuala ya kijeshi nadhani kila nchi ijitegemee, kila nchi ina nguvu yake hakuna taifa dogo kijeshi, kwa hiyo ningependa kumuonya (Trump) awe makini,“amesema Rais Mugabe kwenye mahojiano yake na gazeti la kiserikali la Herald newspaper wakati akihutubia wanachama wa Chama tawala cha Zanu-PF waliojitokeza kumpokea.
No comments:
Post a Comment