Na. Tiganya Vincent – RS-Tabora
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
katika Manispaa ya Tabora inahitaji jumla ya shilingi bilioni 15 kwa
ajili ya hatua za awali za ujenzi wa mtandao wa kuondoa maji taka katika
maeneo mbalimbali mjini humo.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA, Bwire
Mkama wakati wa uzinduzi wa
Malipo kabla ya matumizi ya maji ili kukabiliana na wadaiwa sugu na
wateja ambao upenda kutumia maji bila kulipia huduma hiyo kwa wakati.
Alisema kuwa lengo ni kutaka kuwa
na miundo mbinu itakayosaidia kuondoa maji taka katika majumba ya watu
na mitaa kwa ajili ya kupeleka sehemu ambayo yatawekwa pamoja ili
kuiepushia jamii na maradhi yanaweza kusababishwa na kuzagaa kwa maji
hayo.
Bwire alisema kuwa Bodi ya TUWASA iliona umuhimu kwa kuanza mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya shughuli hiyo.
Alisema kuwa hivi sasa
wameshaandika andiko la uwekezaji katika mtandao wa maji taka na
kulipeleka Wizarani kwa ajili ya kutafuta fedha za kutekeleza mradi huo.
Bwire alisema kuwa wameamua
kuchukua hatua hiyo mapema kwa sababu upatikanaji wa maji safi na salama
unapoongezeka katika miji ndivyo maji taka nayo yanavyoongezeka.
Alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora
kusaidia kusukuma andiko lao ili fedha ya utekelezaji wa mradi huo iweze
kupatikana na kazi ianze mara moja.
Alisema kuwa hivi sasa TUWASA ina
jumla ya kilometa 20 tu za mtandao wa maji taka katikati ya mji wa
Tabora ambapo ni asilimia 6 tu ya wakazi wa Manispaa ya Tabora ndio
wameunganishwa katika huduma hiyo.
Aidha alisema kuwa hivi sasa
wanashirikiana na Manispaa ya Tabora ili kuanisha maeneo ambayo wanaweza
kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji taka.
Kwa mujibu wa Bwire, mabwawa yaliyopo hivi sasa hajatoshi kutokan na ongezeko kubwa la uzalishaji wa maji taka.
Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Aggrey Mwanri alikubali kushirikiana na TUWASA katika
kuhakikisha andiko hilo linafanikiwa na mradi unaanza ili kuboresha
huduma hiyo na kuepusha jamii na magonjwa.
No comments:
Post a Comment